Waziri Silaa amaliza mgogoro wa mpaka kati ya Makete na Wanging’ombe
November 23, 2023, 12:24 pm
Kutokana na kudumu kwa muda mrefu kuhusu mpaka kati ya Makete na Wanging’ombe imetafutiwa ufumbuzi wa tatizo hilo ambao ulikuwa kizungumkuti.
na Gift kyando
Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi mh Jerry Silaha hii leo ametatua mgogoro wa mpaka kati ya wilaya ya makete na wanging’ombe na kutekeleza agizo lililotolewa na makamu wa rais dk fillipo mpango alilolitoa mwezi octabar alipotembelea wilaya ya makete
baadhi ya viongozi wa seriakali na chama katika eneo la mpaka
Akizungumza na wananchi waliokusanyika kwenye viwanja vya shule ya secondary Mount kipengere mh silaha amesema utatuzi huo umehusisha wataalamu kutoka wizara hiyo na hivyo maelekezo alio yatoa kuhusu mpaka halisi yamezingatia utaalamu na uhalisia wa mpaka huo toka awali na sio mapendekezo ya mtu mmoja
Katika hatua nyingine mh silaha amesema serikali itahakikisha inarudia upimaji wa baadhi ya vijiji kwa kuzingatia matangazo ya mipaka ya wilaya kwa kuwa upimaji wa mwanzo haukuzingatia mipaka ya matangazo ya serikali na kujikuta kijiji kimegawanyika maeneo mawili yaani wilaya ya makete na wangingo;mbe huku akisistiza kuwa serikali pia inapendekeza uwepo wa mikutano ya mara kwa mara ya ujirani mwema inayo husisha viongozi wa ngazi zote wilaya kata hadi vijiji
waziri Dkt silaa
Wakizungumza kwa niaba ya wananchi bitrice kyando kutoka makete na musa aldo sanga kutoka wangingo’mbe wamemshukuru mh waziri kwa kufika eneo hilo lenye mgogoro na kutoa maelekezo ya kitaalamu na kutatua Mgogoro huo wa mpaka uliopo karibu kabisa na njia panda ya kuingilia kijiji cha makangarawe
sauti za wananchi
Mkuu wa mkoa wa Njombe mh Antony Mtaka Akitoa shukrani za mkoa kwenda kwa waziri huyo ameomba utekelezaji wa zoezi la upimaji upya kwenye baadhi ya vijiji vilivyo gawanyika maeneo mawili ukamilike mapema ili wananchi wasiwe katika shida ya mipaka ya vijiji baadhi katika eneo hilo la mpka