Dkt Mpango azindua mtambo wa kuzalisha umeme ijangala wenye kilowati 360
November 1, 2023, 11:27 am
Hivi karibuni Makamu wa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mh Philipo Mpango alizindua mtambo wa kuzalisha umeme ijangala wenye kilowati 360
kutokana na umuhimu wa umeme katika shughuli mbali mbali na wengi wao kujiajiri kupitia umeme wadau mbali mbali na serikali wameendelea kushirikiana ili kuweza kufanikisha umeme unawafikia wananchi ili kujikwamua kiuchumi
Na Rose njinile
Hata hivyo Makamu Wa Rais dk philipo mpango mara baada ya uzinguzi huo amesema kuwa kupiitia ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2020 inaendelea kuimarisha sekta ya nishati ili kuweza kupata umeme wa kutosha na kukidhi mahitaji ya uchumi wa viwanda na soko la nje
Aidha Makam wa Rais amesema kuwa kupitia mradi huo wa kufua umeme ijangala utasaidia Shughuli mbali mbali za kujiajiri pamoja na kuwezesha kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia pampu za mashine za umeme
Akisoma Taarifa ya mradi Askofu mkuu wa Dayosisi ya Kusini kati Wilson Sanga amesema kuwa dhumuni kubwa la mradi huo ni kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha upatikanaji wa nishati ya umeme kwa maendeleo ya viwanda vidogo vidogo,ufanisi wa huduma katika taasisi za kijamii pamoja na matumizi ya majumbani
Aidha Askofu Sanga ameipongeza Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuwapa fursa ya ujenzi wa mradi huo utakao chochea maendeleo kwa Taifa la Tanzania
NAE Naibu Waziri wa Nishati mh Judith Kapinga Amelipongeza kanisa la Kkkt dayosisi ya Kusini kati kwa mradi huo na kuongeza kuwa Wizara itaendelea kuthamini juhudi zinazofanywa na wadau wa maendeleo katika kuongeza upatikanaji wa umeme
Mradi huo ulio chini ya kanisa la KKKT umegharimu zaidi ya bilioni tatu mpaka sasa na upo katika Kijiji cha Masisiwe kata ya Ukwama