Askofu Shoo awataka waumini Makete kuungana ujenzi wa kanisa
October 28, 2023, 3:52 pm
Askofu mkuu wa wa kanisa la kilutheri Tanzania Fredrick Shoo pamoja na askofu mkuu wa dayosisi ya kusini ya kati wilson sanga kwenye uwekaji wa jiwe la msingi.picha na Rose njinile
Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu, unaweza kusema hivyo baada ya wananchi kutoka makete na wadau kutakiwa kuungana katika kufanikisha ujenzi wa hekaru la mwenyezi Mungu.
Na Rose njinile.
Inakadiliwa kuwa jumla ya zaidi ya shilingi bilioni moja zinahitajika katika kukamilisha ujenzi wa kanisa kuu la dayosisi ya kusini kati makete mjini
Hayo yamesemwa kwenye zoezi la uwekaji jiwe la msingi katika kanisa kuu la dayosisi ya kusini kati zoezi ambalo limefanyika na mkuu wa kanisa la kilutheri Tanzania dkt Fredrick shoo
Akisoma taarifa ya ujenzi huo katibu mkuu wa dayosisi ya kusini kati mch Ezekiel Sanga amesema kuwa kutokana na changamoto mbali mbali wanazokumbana nazo katika kufanikisha ujenzi huo unakamilika mpaka sasa mradi huo umegharimu zaidi ya shilingi milioni 400
Muonekano wa ujenzi wa kanisa jipya la dayosisi ya kusini kati Makete mjini
Akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi askofu mkuu wa kanisa la kilutheri Tanzania Fredrik shoo amewataka wanamakete kuungana katika kufanikisha zoezi hilo la ujenzi Unakamilika
Nae askofu mkuu wa KKKM kutoka nchi jirani ya Malawi MSUKU ambaye nae alikuwa katika zoezi hilo ameipongeza serikali kwa maendelo yanayofanyika katika wilaya ya makete pamoja na maendeleo ya kujenga hekaru la mungu
Baadhi ya Maaskofu wakiwa na mkuu wa kanisa la kilutheri Tanzania Fredrick Shoo kwenye uwekaji jiwe la msingi
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya makete mh juma sweda amewaomba wanamakete kushirikiana katika kufanikisha ujenzi wa kanisa hilo huku akimshukuru baba askofu Fredrick shoo kufika makete
Aidha nao baadhi ya washirika waliofika katika kushuhudia zoezi hilo la uwekaji wa jiwe la msingi akiwemo aida chengula wamempongeza mkuu wa kanisa la kilutheri Tanzania Fredrick shoo kufika na kufanikisha zoezi hilo huku wakiwataka wanamakete walioko nje ya makete kuweza kufanikisha zoezi la ujenzi linakamilika
Hata hivyo zoezi hilo la uwekaji jiwe la msingi kanisa kuu la dayosisi ya kusini kati umeshuhudiwa na baadhi ya waumini wa kanisa hilo