Kiwanda cha mipira ya kuvaa mikononi (gloves) chazinduliwa rasmi mkoani Njombe
October 28, 2023, 10:08 am
katika kurahisisha upatikanaji wa mipira ya kuvaa mikononi (groves) mkoa wa njombe umekua mstari wa mbele katika kukuza sekta ya afya kwa kuanza na ujenzi wa kiwanda hicho kilichopo katika Halmashauri ya Mji wa Makambako
Na mwandishi wetu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango, Oktoba 26,2023 ametoa maelekezo kwa wizara ya afya pamoja na Bohari ya Dawa Tanzania MSD kuhakikisha inasimamia kiwanda chakuzalisha mipira ya mkono (gloves) mjini Makambako, kinaanza kufanya kazi ifikapo Januari Mosi 2024.
Akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye kiwanda hicho Dkt. Mpango amesema serikali iliamua Kuja na Mpango wa kujenga viwanda kwenye sekta ya afya ili kupunguza uagizwaji wa dawa kutoka nje ya nchi.
Amesisitiza kuwa serikali ilikabidhi jukumu la kuzalisha, kununua, kutunza na kusambaza kwa bohari ya dawa Tanzania MSD ili kuongeza upatikanaji wa vifaa tiba kupungiza matumizi ya fedha kigeni pamoja na kuongeza soko la ajira kwa wa Tanzania.
Aidha ameigiza kuongezwa kwa idadi ya wafanyakazi kwenye kiwanda hicho hasa wanawake wanaotokea kijiji cha Idofi ili waweze kunufaika na mradi huo.
Katika hatua nyingine Dkt Mpango amewataka watumishi wa Bohari ya dawa kuwa wazalendo nakuzingatika maadili ya utumishi.
Kufutia ombi la kuwekwa lami barabara inayoelekea kiwandani hapo lililowasiliswa na Mbunge wa Makambako Mheshimiwa Deo Sanga, Mheshimiwa Dkt Mpango amesema;
Pamoja na hilo ameita MSD kuzingatia misingi ya kibiashara ili iweze kujitegemea kwenye uzalishaji sambamba na kuhakikisha kiwanda cha Idofi kinazalisha bidhaa nyingine kama dawa na vitendnishi.
Aidha ameigiza kundaliwa kwa taarifa ya kina ya mitambo iliyopo kiwandani hapo ambayo haifanyi kazi kwa miaka miwili sasa samba samba na mkakati wa kujibu na kumaliza hoja za ukaguzi.