Wananchi watakiwa kuwa makini na matangazo ya biashara ya dawa, vifaa tiba
October 17, 2023, 1:16 pm
Kutokana na wafanyabiashara kutumia matangazo kufanya bidhaa yake ijulikane na kushawishi watumiaji kutumia bidhaa hiyo TMDA inahakikisha matangazo hayo yanayohusiana na dawa, vifaa tiba na vitendanishi hayana taarifa za upotoshaji.
Na Rose Njinile
Wito umetolewa kwa wananchi wilayani Makete mkoani Njombe kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) pale wanapoona au kusikia tangazo la biashara ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi lenye taarifa zisizo za kweli au zinazolenga kupotosha umma ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa mapema.
Grace Kapande na Adamu Salota ni wakaguzi kutoka TMDA Kanda ya Nyada za Juu Kusini wakizungumza na Kitulo Fm wamesema kuwa lengo la kudhibiti matangazo hayo ni kuhakikisha matangazo yanayohusisana na dawa, vifaa tiba na vitendanishi hayana taarifa za upotoshaji.
Sauti ya Grace na Adamu Salota
Aidha wamesema kuwa kila mwananchi analo jukumu kubwa la kudhibiti matangazo ya dawa ambayo yanaupotoshaji kwenye mamlaka husika pale anapoona kuhisi au kusikia tangazo ambalo lina upotoshaji ndani yake kwa bidhaa zinazodhibitiwa na mamlaka.
Sauti ya grace na admu kutoka mamlaka ya dawa,vifaa tiba
Wakati huo huo Grace Kapande ametoa wito kwa vyombo vya habari hususani kutoka Nyanda za Juu Kusini na Tanzania kwa ujumla kuhakikisha matangazo yanayoletwa hayana upotoshaji na yana kibali
Ikumbukwe kuwa TMDA ni taasisi ya serikali Iliyo chini ya Wizara ya Afya, inayosimamia udhibiti wa ubora, usalama na ufanisi wa dawa, vifaa, tiba na vitendanishi nchini.