Wito watolewa kuwa na desturi ya kujiendeleza na elimu ya watu wazima
October 7, 2023, 9:53 am
Elimu ya watu wazima imeelezwa kua mkombozi kwa watanzania hususani ambao hawakupata nafasi ya kuendele na masomo wakiwa katika mafumo rasmi wa Elim katika Shule za sekondari na Vyuo
na Gift Kyando
Afisa Elimu watu wazima mkoa wa Njombe Joseph A. Lupogo amewataka wazazi na walezi Wilayani Makete kutumia na kuvitunza vituo vinavyotoa elimu kwa ngazi zote ili wenye uhitaji wa kupata elimu wapate elimu na sio kudharau vituo hivyo kwani waanjilishi wa vituo hivyo hulenga kutoa elimu na si vinginevyo
Ameyasema hayo octoba 4,2023 kwenye maadhimisho ya juma la elimu ya watu wazima yaliofanyika Kimkoa Wilaya ya Makete Shule ya Sekondari Iwawa.
Lupogo amesema ipo dhana potofu kwa baadhi ya wanajamii kuona kama Elimu inayotolewa na vituo hivyo haina ubora akichukulia mfano kituo cha jitambue jambo ambalo halina ukweli.
Katika hatua nyingine ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Makete kwa kuanzisha vituo vinavyotoa elimu ya watu wazima kwa ufasaha kwani hilo linaonyesha namna ambavyo viongozi wa wilaya na jamii wanavyo tambua umhimu wa elimu kwa ngazi zote
Kwa upande wake Afisa Elimu watu wazima Wilaya ya Makete ndg Baptista Kaguo amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeboresha mazingira ya kujifunza kusoma ,kuandika na kuhesabu kwa kuzingatia ubora na usawa ikijumuisha makundi yote kwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Makete jumla ya wanafunzi 3 waliosoma elimu nje na mfumo rasmi walifaulu mitihani ya darasa la nne na kujiunga na mfumo rasmi
Sanjari na hilo wanafunzi 13 waliocheleweshwa kuanza darasa kwanza wameandikishwa kwenye shule mbali mbali za msingi zenye vituo 8 vya MEMKWA
kaguo Amesema vituo hivyo vinavyo toa elimu ya MEMKWA katika Wilaya ya Makete vipo katika shule za msingi za Matamba , Bulongwa, Lupombwe, Ivalalila, Mlondwe , Ikuwo, Sunji na Mang’oto na kuongeza kuwa kwenye maeneo ambako hakuna vituo hivyo walengwa hujiunga na kwenye shule yeyote ya msingi ya Serikali au binafsi na hufundishwa na wanafunzi wengine kwani shule zote za msingi ni vituo vya elimu ya watu wazima
Maadhimisho ya kilele cha juma la Elimu ya watu wazimu Kitaifa yatafanyika tarehe 9 Octoba na kauli mbiu ya maadhimisho haya ni kukuza uwezo wa kusoma na kuandika kwa ulimwengu unaobadilika, kujenga misingi ya jamii endelevu na yenye amani