Wahitim 34 watunukiwa vyeti shule ya sekondari Kitulo
October 7, 2023, 9:31 am
Kuelekea mtihani wa Taifa wa kumaliza elimu ya sekondari jumla ya wanafunzai 34 wametunukiwa vyeti vya kuhitimu elimu ya sekondari katika shule ya sekondari Kitulo iliyopo Makete Njombe
na Aldo Sanga
Jumla ya wanafunzi 34 wa metunukiwa cheti cha kuhitim masomo ya kidato cha nne katika maafari ya 12 katika shule ya sekondari kitulo,
Akikabidhi vyeti vya kuhitim elimu ya sekondari Mh:Abeli Mahenge diwani wa kata ya kitulo ambaye ndiye alikua mgeni rasmi amewapongeza vijana hao kwa kuvumilia katika masomo yao huku akiwataka kutia nia katika kuyafikia malengo yao
Mh:Mahenge ameongeza kua chanagamoto zilizoelezwa hasa katika kuboresha na kuongeza miundombinu ya shule hususani katika majengo Halmashauli ya Wilaya kupitia mpango wa maendeleo TASAF Imetoa fedha na tayari ujenzi wa bweni umeshafikia hatua za umaliziaji hata hivyo ameahidi kuziwasilisha katika ngazi husika
Mwl, Degdus Ezekiel Mwatujelele ni makam mkuu wa shule ya sekondari kitulo kwaniaba ya mkuu wa shule ameeleza mafanikio ya shule kua nipamoja na ongezeko wa ufaulu katika shule ambapo katika mitihani ya kujipima baadhi ya wanafunzi walifanya vizuri mwanafunzi mmoja kutoka shule ya kitulo alishika nafasi ya kwanza na wapili nafasi ya tatu kiwilaya katika matokeo ya kidato cha pili huku akiongeza kua mafanikio hayo yametokana na ushirikiano wa walimu serikali pamoja na wazazi,
Shule ya sekondari kitulo nimiongoni mwa shule zilizopo katika wilaya ya Makete karibu na hifadhi ya Taifa ya kitulo yenye jumla ya wanafunzi 186 hadi sasa imesha fanya maafari 12 tangu kuanzishwa kwake.