Kitulo FM
Kitulo FM
October 5, 2023, 8:52 am

Kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Matamba serikali imetoa fedha shilingi milioni 700 kutatua changamoto hiyo,
Na mwandishi wetu.
Fedha hizo zimetumika kujenga vyumba 8 vya madarasa, bweni 4 na vyoo matundu 13.
Madarasa, vyoo na mabweni matatu yamekamilika kwa fedha za Serikali Kuu huku bweni moja linalojengwa kwa fedha za SEQUIP likiwa hatua ya kupandisha kuta.