Kitulo FM

Serikali yatoa fedha ukarabati wa hospitali ya wilaya Makete

October 2, 2023, 8:53 am

Mwonekano wa jengo la huduma za dharula. Picha na Furahisha Nundu

Kupitia uchakavu wa Hospitali ya wilaya ya Makete serikali umetoa fedha zaidi ya shilingi milioni miatisa (900) kukarabati miundombinu ikiwemo Majengo

Majengo makubwa matano (5) yamejengwa Hospitali ya Wilaya ya Makete kwa fedha za Serikali zaidi ya shilingi Milioni 900 na kuboresha miundombinu ya Hospitali hiyo ambayo majengo yake yalikuwa chakavu

Majengo yaliyojengwa kwa fedha hizo ni Jengo la Upasuaji, Maabara, Jengo la kufulia, Kichomea taka cha Kisasa (High Tech) na ukarabati wa Jengo la Wagonjwa wa nje (OPD) ambapo majengo yote yamefikia zaidi ya 95%

Katika Taarifa yake Kwa Kamati ya Siasa (CCM) Mkoa wa Njombe, Mganga mfawidhi Hospitali ya Wilaya Ndg. Jonathan Kitundu amesema kukamilika kwa uboreshaji wa miundombinu hiyo kutaboresha utoaji wa huduma wezeshi za Afya kwa kupunguza gharama za matibabu kwa Wananchi

daktari Jonathani Kitundu akitoa maelezo hatua ya utekelezaji wa maradi kwa mwenyekiti wa kamati ya siasa mkoa wa Njombe Deo Sanga. picha na Furahisha Nundu

Pia kupunguza vifo vya wagonjwa yanayohitaji huduma za dharula, kuwezesha watoahuduma kutoa huduma katika Mazingira rafiki na uwepo wa Vifaa Tiba vya kitosha, kuwezesha ufungaji wa Vifaa vya Kisasa na kuongeza mwitikio wa Wananchi wanaofika kupata huduma katika Hospitali ya Wilaya

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe (Mb) Mhe. Deo Sanga akizungumza na Wananchi wa Iwawa ilipo Hospitali hiyo amewasihi kujitokeza kupata huduma za Afya katika Hospitali hiyo kwani Serikali inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha miundombinu ya upatikanaji wa huduma bora kwa Wananchi wake.

Mbunge Jimbo la Makete Mhe. Festo Sanga amesema pamoja na fedha hizo kutolewa Bado Serikali imetoa fedha zaidi ya Bilioni 2 kujenga Jengo la Halmashauri ya Wilaya huku fedha za Ujenzi wa Madarasa katika maeneo mbalimbali Wilayani Makete zikitolewa ikiwa ni pamoja na ufungaji wa Taa za Barabarani eneo la Makete Mjini

Diwani Kata ya Iwawa Mhe. Fransis Chaula amesema Serikali imekarabati zaidi ya Km. 10 za Barabara ya Kokoto katika maeneo mbalimbali ya Iwawa, Madarasa yamejengwa, Usambazaji wa Umeme umefanyika na Miradi ya Maji inaendelea kutekelezwa katika Mji mdogo wa Iwawa.

Eng:Maganga akielezea hatua ya utekelazaji wa mradai.picha na Furahisha Nundu