Miundombinu shule ya sekondari ya wasichana Makete sasa shwari
October 2, 2023, 8:32 am
Kupitia ongezeko la wanafunzi hususani kidato cha tano na cha sita serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa fedha kiasi cha shilingi bilioni 1 kujenga madarasa shule ya sekondari ya wasichana Makete.
na Furahisha Nundu
Kiasi cha shilingi bilioni moja na milioni 50 zimetolewa na serikali kwa ajili ya kujenga madarasa, bweni na vyoo shule ya sekondari ya wasichana Makete.
Fedha hizo zimetolewa kupitia miradi ya EP4R kwa ajili ya upanuzi wa miundombinu katika shule hiyo ikiwa ni miundombinu kwa ajili ya kidato cha tano na cha sita ikiwemo madarasa 10, vyoo matundu 10 na mabweni matano.
Kwa mujibu wa mkuu wa shule hiyo Mwl. Sayuni Sanga amesema ujenzi wa vyumba 10 vya madarasa umekamilika huku akiongeza kuwa ujenzi wa vyoo na bweni upo katika hatua za mwisho.
Shule la sekondari ya wasichana Makete ina jumla ya wanafunzi 607 kidato cha kwanza hadi kidato cha sita.