TADIO yawapiga msasa waandishi Kitulo FM
September 23, 2023, 3:41 pm
katika mwendelezo wa kuwajengea uwezo wanahabari juu ya matumizi ya redio mtandao mtandao wa redio jamii Tanzanio wametoa mafunzo katika kituo cha redio Kitulo FM huki waanahabari wakisisitizwa kutumia habari za kijamii na kua wabunifu katika uandishi wa habari
Na Furahisha Nundu
Mtandao wa Redio Jamii nchini (TADIO) umefanya mafunzo ya ndani kwa waandishi wa habari wa kituo cha jamii Kitulo FM.
Mafunzo hayo ya siku moja yametolewa leo Septemba 23, 2023 na Ndugu Amua Rushita kutoka TADIO kwa lengo la kukumbushana maadili ya uandishi wa habari na matumizi sahihi ya kusambaza habari katika mitandao ya kijamii.
Waandishi hao wamesisitizwa pia kuendana na kasi ya matumizi ya mitandao ya kijamii kusambaza taarifa ikiwemo matumizi ya jukwaa la habari za radio jamii Tanzania www.radiotadio.go.tz
“Tutumie Ukurasa huu wa radio TADIO kutoa na kusambaza taarifa mbalimbali zinazohusu jamii yetu kwani mitandao ya kjamii ina nguvu kubwa katika ulimwengu huu na tuhakikishe tunazingatia weledi wa taaluma yetu” amesisitiza Rushita.
Kituo cha redio Kitulo FM kinamilikiwa na halmashauri ya wilaya ya Makete kikiwa na wafanyakazi 8 na kinajikita kutoa habari za ndani ya wilaya na nje ya wilaya.