wakulima wahimizwa kuhuisha taarifa zao kwenye daftari la wakulima
September 12, 2023, 10:29 am
kulingana na serikali kutoa ruzuku ya pembejeo wakulima wametakiwa kuendelea kuhuisha taarifa zao kwenye daftari kwa wakati ili kuepuka usumbufu wa kupata pembejeo
na mwandishi wetu
Wakulima Wilayani Makete Mkoani Njombe wametakiwa kwenda kwenye Ofisi za Vijiji ili kuhuisha taarifa zao kwenye Daftari la wakulima
amesema kwa msimu wa kilimo 2023/24 wakulima wameanza kuandikishwa kwenye daftari la wakulima ili waweze kupata pembejeo za kilimo kwa bei ya ruzuku
Akizungumza na Kitulo FM Leo Septemba 5, 2023 Mtaalamu kutoka Idara ya kilimo, Mifugo na Uvuvi Wilaya ya Makete Ahmed Kichombaki amesema kwa msimu wa kilimo 2023/24 wakulima wameanza kuandikishwa kwenye daftari la wakulima ili waweze kupata pembejeo za kilimo kwa bei ya ruzuku
Kichombaki ameelezea changamoto ya wakulima kuwa na mwitikio mdogo wa kujiandikisha na kuwasihi wajitokeze kwa wingi ili kufanikisha zoezi hilo
Afisa Takwimu na pembejeo Wilaya ya Makete Ndg. Mnyama Charles amesema dirisha la usajili lilianza Septemba mosi na linatarajiwa kufungwa tarehe 15 Septemba, 2023
Msimu wa kilimo 2023/24 umeanza wilayani makete ambapo wakulima wamekuwa wakinufaika na pembejeo za ruzuku kutoka serikali kwa bei ya punguzo kutoka laki moja na nusu hadi elfu sabini.