Tuulinde Utamaduni wetu-Waziri Balozi Dkt. Pindi
August 27, 2023, 8:28 pm
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema utamaduni unaodumishwa katika Taifa umesaidia kudumisha Amani tofauti na Mataifa mengine.
Waziri Pindi Chana ametoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Kitaifa la Utamaduni linalofanyika Mkoani Njombe na kwamba Wizara imeendelea kuwa chachu ya kudumisha Amani na kutoa ajira nyingi kwa Vijana.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara hiyo Saidi Yakubu amesema maagizo ya Rais ya kufanyika kwa Matamasha ya utamaduni kunasaidia kuunganisha makabila yote Tanzania bara na Visiwani ikiwa ni moja ya njia kurahisisha udumishaji wa mila za kiafrika.
Mwenyekiti wa Umoja wa Machifu Tanzania Antonia Sangalai amesema tamaduni za kiafrika ni muhimu kuenziwa kwa kuwa zinasaidia kukabiliana na changamoto ya mmomonyoko wa maadili.
Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe. Kissa Gwakisa amesema wakati Tamasha likiendelea wananchi wamekuwa wakidumisha utamaduni pamoja na kufanya kazi kwa bidii
Baadhi ya wakazi wa Njombe akiwepo Rashidi Karume, na Ulaya Kayombo wamesema Tamasha hilo litawafungulia milango ya kiuchumii huku wengine wakionya kutorithi utamaduni mbaya za mataifa ya kimagharibi