BAKITA yawanoa Waandishi wa Habari Njombe Matumizi Sahihi ya Kiswahili
August 26, 2023, 12:46 pm
Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) limetoa elimu kuhusu Matumizi sahihi ya Lugha ya Kiswahili kwa Waandishi wa Habari na Maafisa Habari Mkoa wa Njombe
Huu ni katika kuhakikisha Matumizi ya Lugha kwa Wanahabari katika maeneo yao ya kazi na kuongeza chachu ya Matumizi sahihi ya Kiswahili kwa Wananchi kupitia vyombo vya Habari.
Mhariri Mwandamizi kutoka BAKITA Ndugu Onni Sigala Maudhui yanayotolewa kwa walaji kupitia burudani, Habari kuwa fasaha na sanifu kwani Vyombo vya habari visipotumia Lugha Fasaha inaweza kupotosha Jamii au kudobosha habari nzito na makini ambayo ilimefikiwa kwa Jamii, hivyo kushusha thamani ya maudhui ambayo yamekusudiwa kuwafikia walengwa
Mhariri Mwandamizi BAKITA Onni Sigala amesema kumekuwa na makosa mengi yanayofanywa na Wanahabari katika maudhui yanayotolewa kupitia vyombo husika vya habari na kusababisha kutoonyesha umakini na adabu kwa Mtazamaji, Msikilizaji au msomaji kwa kutotumia tafsida/Lugha ya kificho katika mambo ya Kijamii.
“Sisi kama Wanahabari tunapaswa kuzingatia Utamaduni wa Jamii yetu na walengwa wanaopata habari wakati wote wa upashanaji wa Habari kwa Jamii bila kuwanyima taarifa kwani kufanya hivyo ni kutotenda haki ya kupata na kutoa taarifa”.
Katibu Mtendaji BAKITA Bi. Consolata Mushi amewasihi waandishi wa Habari kufanya utafiti wa taarifa kwa umakini ili kutobebesha baadhi ya misamiati isiyo sahihi katika taarifa zinazotolewa kupitia Redio, Televisheni, Magazeti na hata mitandao ya Kijamii
Bi. Mushi amesema ni vema waandishi wa Habari wakajikita katika kuongeza umakini kwenye uandishi, utamkaji wa maneno na Uhariri huku akiwasihi wanahabari kuteua maneno ya kutoa kwa Jamii kulingana na ufasaha wa Lugha
“Waandishi wa Habari ni nyenzo muhimu ya kukuza Kiswahili ndani ya Tanzania na Mataifa ya nje kupitia taaluma mliyonayo ambayo inaweza kuwa njia rahisi ya kubidhaisha Lugha yetu”
“Waandishi wa Habari mnafuatiliwa na watu wengi kwa muda mfupi na hii inasababisha watu kupata taarifa kwa haraka zaidi kuliko mtu yeyote…mnapaswa kusaidia ukuzaji wa Lugha kwa kutumia maneno sahihi”