Wananchi vijiji 44 kupewa hati za kimila bure Makete
June 26, 2023, 7:16 am
Halmashauri ya wilaya ya Makete kwa kushirikiana na tume ya taifa ya mipango ya matumizi bora ya ardhi imeanza kutoa elimu ya mpango wa matumizi ya ardhi katika vijiji 44 katika kata za Ikuwo, Kigala, Kinyika, Iniho, Kipagalo, Luwumbu, Bulongwa, Ipelele, Matamba, Mlondwe na Itundu.
Akizungumza na kwenye mkutano wa utoaji elimu ya mpango wa matumizi bora ya ardhi na wananchi wa kijiji cha Mpangala kata ya Matamba, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Makete William Makufwe amesema halmashauari kwa kushirikiana na tume ya taifa ya mipango ya matumizi bora ya ardhi wamelenga kuwasaidia wananchi upatikanaji wa hati za hakimiliki za kimila bure kwenye mashamba yao kwa ajili ya kukuza kilimo cha ngano na uchumi wa wananchi wa Makete.
Zoezi hilo limeanza tarehe 16 Juni 2023 katika vijiji mbalimbali ambapo mwitikio wa wananchi umekuwa mkubwa huku wakikubaliana maeneo yote yapimwe ili kuwa na mpango bora wa matumizi ya ardhi kwenye vijiji vyao.
Mkurugenzi Mtendaji H/W ya Makete William M. Makufwe akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mpangala kwenye Mkutano wa kuelezea umuhimu wa ardhi yao kuwa na Hati.