Mapokezi ya Jokofu la kuhifadhia Maiti Hospitali ya Wilaya ya Makete
Kitulo FM

Hospitali wilaya Makete yapokea jokofu la kuhifadhia maiti

June 21, 2023, 7:47 am

Hospitali ya wilaya ya Makete imepokea jokofu la kuhifadhia maiti 6 kwa wakati mmoja.

Jokofu hilo limepokelewa leo baada ya kuletwa na serikali ambapo hospitali haijawahi kuwa na jokofu kwa ajili ya kuhifadhia watu waliofariki.

Mganga Mkuu wa hospitali ya wilaya Jonathani Kitundu akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu wilaya ya Makete ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusaidia upatikanaji wa jokofu hilo.