Dawa za P2 si kila mtu anapaswa kuitumia
June 9, 2023, 7:51 am
Dawa aina ya P2 zimetengenezwa kwa ajili ya kumsaidia mama au binti kutopata ujauzito ambao hakutarajia na dawa hii ni aina ya uzazi wa mpango inayotumika wakati wa dharura.
Dharura hizo kwa mwanamke kushiriki tendo la ndoa katika siku ambazo ni hatarishi kwakwe kupata ujauzito kwa mfano kondom kupasuka, pindi mwanamke anapotumia njia ya kalenda na amekosea kuhesabu ama mwanamke aliyebakwa.
Uwepo wa dawa hizi umekuwa na msaada kwa wanawake ama mabinti ingawa kwa sasa umekuwa na madhara makubwa kwa baadhi ya watumiaji kutokana na matumizi holela ya dawa hizi. Hapa mkaguzi wa dawa na vifaa tiba kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) Jofrey Kikoti anaeleza madhara hayo;
Bi. Krace Kapande ambaye ni mkaguzi wa dawa na vifaa tiba ameeleza hatua ambazo zinachukuliwa na TMDA baada ya tathmini ya madhara ya matumizi holela ya P2 ikiwemo kuishauri Wizara ya Afya kubadilisha sera ya dawa husika ndani ya nchi.
TMDA ni taasisi iliyo chini ya Wizra ya Afya inayosimamia udhibiti wa ubora , usalama na ufanisi wa dawa, vifaa tiba na vitenganishi nchini , mamlaka hii imeundwa chini ya sheria ya dawa na vifaa tiba sura ya 219.