Wanawake waaswa kutumia Teknolojia
March 9, 2023, 10:44 am
Wanawake Wilayani Makete Mkoani Njombe wameiomba Serikali kuendelea kupambana na ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya wanawake na kukosekana kwa haki kutaendelea kupelekea kushindwa kuwa wabunifu na kuendana na mabadiliko ya Teknolojia.
Akisoma risala kwa niaba ya Wanawake wa Wilayani hapa Mch Lea Sowo amesema unyanyasaji wa kijinsia umekuwa ni changamoto katika jamii ya wanawake huku baadhi ya wanaume wakikwepa majukumu ya kifamilia ikiwemo kupeleka watoto Shuleni.
Akijibu risala hiyo Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete Bi. Grace Mgeni amesema, ili mwanamke aweze kutimiza ndoto zake anatakiwa apewe nafasi tangu akiwa mtoto ikiwemo kupata Elimu kwani kufanya hivyo kutafanya kufikia kizazi chenye usawa huku akiwapongeza wanamakete kwa kuwapa nasafasi watoto wa kike katika kupata elimu.
Bi. Grace amewapongeza wanawake kwa kubeba majukumu ya kifamilia na kujihusisha na shughuli za kilimo kuhakikisha upatikanaji wa chakula na kuongeza kipato katika familia huku akiitaka jamii kuchukua jukumu la kumsaidia mwanamke na amewataka wanawake kujitambua kuwa wanahaki sawa katika kumiliki rasilimali.
Ili kufikia mabadiliko ya kiuchumi kwa wanawake ni lazima jamii kubadili fikra na kuleta usawa wa kijinsia kwa kumpunguzia Mwanamke baadhi ya majukumu ikiwemo kulea familia.
Amesema Serikali imekua ikifanya jitahada ili kuwawezesha Wanawake na kuhakikisha kuwa wanashiriki katika masula ya Siasa na kwa uchaguzi uliopita wanawake wamejitokeza katika nafasi za uongozi hii inaonyesha jinsi wananwake wanahitajika katika uongozi huku akiwaasa wanawake kujiunga katika vikundi ili wajipatie mikopo.
Akizungumza kwa niaba ya wanawake Mama Suvile amewaasa wanawake kuacha tabia ya kuwategemea wanaume kwa kila kitu kwa kufanya hivo kunasabaisha ndoa zao kuvunjika na kutoishi kwa mani katika familia zao
Wanawake Kata ya Bulongwa wamefanya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani huku wakiwataka Wazazi na walezi Wilayani Makete wametakiwa kushirikianiana katika kuwalea watoto kwenye maadili mema huku wakitakiwa kuacha tabia ya kuwatorosha watoto kwenda kufanya kazi za ndani. Wakiwa katika maadhimisho hayo Diwani Viti maalumu Tarafa ya Bulongwa Mhe. Joyce Sanga akiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Mwanamke Duniani yaliyofanyika Kata ya Kata ya Bulongwa ambapo amewataka kupeleka watoto shule ili waweze kupata haki yao ya Kimsingi ya kupata Elimu