Polisi Wanawake Makete wawafariji Yatima Bulongwa
March 7, 2023, 9:59 pm
Mtandao wa Jeshi la Polisi Wanawake Wilayani Makete Mkoani Njombe wametembelea kituo cha kulelea watoto Yatima Bulongwa na kutoa msaada wa vitu mbali mbali vyenye thamani ya shilingi laki tatu .
Philipina mkumbo ni Mkuu wa upelelezi Wilaya ya Makete amesema moja ya kazi kubwa wanayofanya wanawake ndani ya Jeshi la Polisi Tanzania ni kusaidia watoto na kuwaona watoto wenye mazingira magumu pamoja na kutoa elimu kwa watoto na hata jamii nzima namna ya kuzuia uhalifu katika maeneo yao
Kwa upande wake Mkuu wa Kituo cha kulelea Watoto Bulongwa Vaileth Chaula amewashukuru mtandao wa Jeshi la Polisi Wanawake Makete kwa kujitoa kwao na kuwatembelea katika kituo hicho
Nao baadhi ya Askari wanawake waliohudhuria katika kituo hicho wamewapongeza walezi wa watoto hao kwa jitihada zao wanazozifanya kuhakikisha watoto wanapata malezi bora
Ikumbukwe kuwa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani hufanyika kila tarehe nane machi ya kila mwaka ambapo kwa mwaka huu maadhimisho hayo yanakwenda sambamba na kauli mbiu isemayo UBUNIFU NA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA, CHACHU KATIKA KULETA USAWA WA KIJINSIA