Kikao Kazi kuelekea Kilimo cha Ngano Makete
March 6, 2023, 6:59 pm
Kikao kazi cha maafisa Ugani na Kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Makete kitakachofanyika kwa siku mbili kimeanza leo katika Mkakati wa kuendeleza zao la Ngano Makete.
Kikao hicho kimehudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo wanafunzi 80 kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) Morogoro, Tari Uyole, ASA, TFRA, na wadau wengine
Hapo kesho siku ya pili ya Kikao kazi hicho Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka anatarajiwa kuhudhuria sambamba na Wadau kutoka Wizara ya Kilimo, Bakhresa Group, NMB, CRDB na Viongozi mbalimbali kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe.
Akiwa katika ufunguzi wa Kikaokazi hicho Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Makete William Makufwe amewaeleza wataalamu hao nia ya Halmashauri kuwasaidia wakulima wa Zao la Ngano Wilayani Makete.
Makufwe amewaelekeza wataalamu hao wa Ugani kusimamia shughuli zote za Kilimo cha Ngano kwa wakulima, kuratibu upatikanaji wa pembejeo zinazohitajika kwa wakulima, huku wakitakiwa kuongeza uwezo rejea ili kuwa na Kilimo chenye tija kwa Mkulima