Ukaguzi wa Miradi
Kitulo FM

Kamati ya Fedha Makete yakagua miradi ya Zaidi yha Bilioni 1.5

February 16, 2023, 1:52 pm

Wajumbe wa Kamati ya Fedha Halmashauri ya Wilaya Makete wametembelea na kukagua miradi mbalimbali yenye zaidi ya thamani ya Bilioni 1.5 katika kata tatu.

Miradi hiyo inatekelezwa na fedha za Serikali katika Kata ya Iwawa, Iniho na Ipelele Wilaya ya Makete

Kamati hiyo ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Hawa Kader, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Albert Msemo, wajumbe (waheshimiwa Madiwani) na wataalamu wamekagua ujenzi wa Madarasa shule ya Msingi Ipelele mradi wa Milioni 250, Nyumba ya Walimu (3 in 1) shule ya Msingi Kilimani Kidope yenye thamani ya Milioni.

Mradi wa Ujenzi wa uzio bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalumu shule ya Msingi Makete kwa Milioni 30, ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi ya walimu Shule ya Sekondari Iwawa mradi wenye thamani ya Milioni 40.

Kamati pia imekagua ukamilishaji wa Vifaa katika Jengo la dharula Hospitali ya Wilaya Makete jengo lililojengwa kwa zaidi ya Milioni 300, na ukarabati wa Hospitali hiyo ambayo Serikali imeshatoa Milioni 900 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi kwa baadhi ya majengo.