Kitulo FM

Watendaji wa Kata simamieni Wanafunzi waende Shule-Dc Sweda

January 29, 2023, 8:42 am

Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda amesema kiwango cha wanafunzi Tarafa ya Ikuwo kuripoti shule ni hafifu

Ameagiza Afisa Tarafa, watendaji wa kata kufanya msako maalumu kuhakikisha wanafunzi ambao hawajaripoti kidato cha kwanza mpaka sasa wanaripoti shule na wazazi watakaokiuka agizo hilo wachukuliwe hatua.

Akizungumza kwenye Baraza maalumu la kupitisha Bajeti ya Maendeleo na mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Mhe. Sweda amesema ni muhimu kuzingatia agizo hilo kwa kuwa hali ya wanafunzi kuripoti shule katika Tarafa ya Ikuwo imekuwa hafifu.