Jengo la Dharula limekamilika na Milioni 900 zimeanza kujenga Hospitali ya Wilaya
January 25, 2023, 12:36 pm
Serikali imekamilisha ujenzi wa Jengo la dharula katika Hospitali ya Wilaya Makete kwa zaidi ya Milioni 300 ambapo tayari vifaa vinefika kwa ajili ya kuanza kutoa huduma.
Kamati ya Siasa Wilaya ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya Clement Ngajilo akiambatana na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Hawa Kader, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Ndg William Makufwe na wajumbe wa Kamati hiyo asubuhi ya leo Januari 24,2023 wamekagua ujenzi wa Jengo la Upasuaji,Maabara, Jengo la kufulia, Kichomea taka na ukarabati wa Jengo la wagonjwa wa nje kwa Milioni 900 fedha kutoka Serikali kuu
Kamati hiyo imepongeza juhudi za Serikali kwa kutoa fedha hizo na usimamizi madhubuti wa ujenzi katika Hospitali hiyo
Mkuu wa Divisheni ya Miundombinu Wilaya Emily Maganga amesema mpaka kufika mwezi wa nne, 2023 majengo hayo yatakuwa yamekamilika kujengwa