Wananchi washangazwa na mto wa Mawe Ipelele
January 24, 2023, 7:03 am
Wananchi wa Kijiji cha Ipelele wameiomba Serikali kuwachia suala la mto unaoporosha mawe kwa zaidi ya Miaka 7 sasa kimaajabu.
Wakizungumza na Kituo hiki, wananchi wa Kijiji cha Makwaranga kilichopo Kata ya Ipelele Wilayani Makete wamesema mto huo wenye maji kidogo ulianza kuporomosha mawe kwa wingi mwaka 2027 ilihali miaka ya nyuma haikuwa hivyo na kusababisha kuzolewa kwa Daraja lililokuwa linaunganisha barabara ya Ipelele-Makwaranga.
Kwa mujibu wa wananchi hao wamesema “Serikali haiamini haya mambo (Uchawi/Mizimu) sasa tunaomba ituachie ili tushughulikie jambo hili” alisema mwananchi mmoja
Kwa sasa Serikali inajenga Daraja kubwa katika eneo hilo lenye thamani ya Zaisi ya Milioni 170 lakini pindi mvua inaponyesha hukusanya mawe mengi na kuporomoka kupitia Daraja hilo huku wakihofia mawe hayo huenda yakabomoa tena daraja hilo.
Mhandisi John Peter Kawogo kutoka TARURA Makete amesema Serikali inajenga Daraja hilo kuhakikisha wananchi hawakosi huduma ya usafiri na Daraja limejengwa kwa viwango kulingana na uhalisia wa mto uliopo kutiririsha mawe kwa wingi kutoka Mlimani.