Kitulo FM

Wajanja wa kurubuni Mbolea kushughulikiwa Njombe

January 19, 2023, 7:53 am

Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka akishirikiana na Jeshi la Polisi mkoani hapa, wamefika katika nyumba ambayo mfanyabiashara wa mbolea amekuwa akitumia kuchakachua bidhaa hiyo.

Mtaka amesema katika nyumba hiyo isiyo na umeme, wamebaini mifuko ya makampuni mbalimbali ya mbolea, majenereta mawili na mashine ya kufungia mifuko, lakini pia wameikuta mifuko yenye mbolea ambapo jina la kampuni halifanani na mbolea iliyo ndani.

Katika hatua za awali Mkuu wa mkoa huo ameagiza Jeshi la Polisi kufanya ukaguzi wa bidhaa hiyo katika maduka ya mfanyabiashara huyo na kufunga maduka hayo hadi upelelezi utakapo kamilika