Wanafunzi walioacha masomo washauriwa kujisajili waanze kusoma
January 16, 2023, 8:24 am
Wanafunzi wa kike walioacha masomo kwa sababu mbalimbali kuanzia mwaka 2016 wametakiwa kujiandikisha ili waweze kuanza masomo kwa muhula wa masomo 2023/24 katika program ya Elimu ya Sekondari kwa Njia Mbadala (SEQUIP-AEP)
Baptista Kaguo Mratibu wa elimu ya watu wazima na Elimu nje ya mfumo usiorasmi akizungumza na Kitulo FM amesema, wanafunzi hao wanastahili kupata elimu bila kujali waliacha masomo kwa kupata ujauzito, ugonjwa na sababu zingine.
Kaguo ameongeza kuwa Serikali imetoa fedha kwa ajili ya kuwasomesha wanafunzi hao kwa muda wa miaka miwili na watahitimu kidato cha nne, huku gharama zote za chakula zikiwa juu ya Serikali kwa muda huo wote.
Mwaka 2022 Mkoa wa Njombe waliandikishwa wanafunzi 120 ambapo Kitaifa waliandikishwa wanafunzi 3,333 sawa na 111%
Masomo yanatarajiwa kuanza tarehe 16 januari katika Kituo cha Makambako, Njombe FDC na Ulembwe