Kitulo FM

Mwanafunzi hata kama hana Sare aanze Masomo-dc Mhe. Sweda

January 7, 2023, 8:32 pm

 

Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda amekagua vyumba vya madarasa kwa shule za Sekondari ambavyo wanafunzi wataripoti na kuanza masomo Januari 9, 2023.

Mhe. Sweda amesema Serikali imehakikisha wanafunzi wanapata Mazingira rafiki ya kujifunzia na hivyo mpaka sasa hakuna sababu ya Mwanafunzi yeyote kusoma masomo bila sababu za Msingi.

 

Mkuu wa Wilaya ya Makete (Katikati) akiwa amekaa kwenye viti vitakavyotumiwa na wanafunzi Kidato cha kwanza kuanzia Januari 9, 2023

Mkuu huyo wa Wilaya amewasihi wazazi kuhakikisha watoto wote waliofaulu na kupangiwa shule za kwenda wanawapeleka wanafunzi hao kwa wakati ili kuepuka mkono wa Sheria.

Ameongeza kuwa endapo Mzazi ameshindwa kumudu vifaa vya mwanafunzi kama Sare na vifaa vingine haviwezi kuzuia mwanafunzi kuanza masomo wakati taratibu za kukamilisha mahitaji yake zikiendelea.

Mwonekano wa Chumba kimoja cha Darasa shule ya Sekondari Lupalilo