Kitulo FM

Miundombinu imekamilika kupokea Wanafunzi Januari 9, 2023- Mhe. Mpete

January 7, 2023, 7:28 pm

 

Mwenyekiti wa Halmashauri mji Njombe Erasto Mpete akizungumza na wanahabari amesema Mazingira yamewekwa sawa kwa ajili ya kupokea wanafunzi

Wakati shule zote nchini Tanzania zikitarajiwa kufunguliwa siku ya Jumatatu ya Januari 9 ,2022 wazazi na walezi mkoani Njombe wametakiwa kuwaandalia watoto mahitaji yote muhimu ili wanafunzi wote waripoti shule na kuanza masomo kwa pamoja.

Akizungumza na wanahabari Mwenyekiti wa Halmashauri mji Njombe Mhe. Erasto Mpete amesema kwa upande wa serikali wamehakikisha miundombinu yote inakamilika kwa wakati ikiwemo Vyumba vya madarasa na Madawati kilichobaki ni wazazi kuwapeleka watoto shule.

Kalmas Konzo ni mwalimu kutoka shule ya Msingi Livingtone iliyopo mkoani Njombe amewaasa wazazi na walezi kutowachelewesha watoto shule kwani kuna madhara makubwa atayapata mtoto huku pia akiwakumbusha wanafunzi kuwa wasahau kuhusu likizo wairejeshe akili kupokea kwenye masomo.