Waziri wa Viwanda anena kuhusu uwekezaji wa Malengo
December 2, 2022, 8:46 pm
Dar es Salaam, Novemba 30, 2022: Jukwaa la kwanza kuwahi kutokea Tanzania la Uwekezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) limefanyika leo Jijini Dar es Salaam na limeratibiwa na UNDP na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara (MIIT) na Mfuko wa Maendeleo ya Mitaji wa Umoja wa Mataifa (UNCDF).
Mgeni Rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa na dhamira ya jukwaa ni “Wekeza Katika Tanzania Ijayo”.
Jukwaa la Uwekezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu Tanzania linalenga dhumuni la kuzindua Ramani ya Mwekezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu Tanzania na kurahisisha mabadilishano ya mawazo kati ya wawekezaji na shughuli/miradi ambayo inaangukia katika maeneo ya fursa za uwekezaji (IOAs).
Jukwaa linalenga kuweka njia ya mabadilishano ya mawazo kuhusu sera ya taifa ya ajenda ya Tanzania kuhamasisha uwekezaji wa malengo ya maendeleo endelevu na kurahisisha maendeleo nchini.