Ahukumiwa Miaka 30 Jela
November 9, 2021, 2:17 pm
Frank sanga (23) mkazi wa iniho Wilayani Makete Mkoani Njombe amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka (13) (jina limehifadhiwa) wa kijiji cha Iniho
Imeelezwa kuwa mnamo tarehe 7 oktoba,2021 katika kijiji cha iniho mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo la kumbaka mtoto huyo wa shule ya msingi iniho ambalo kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 130 (1)(2e)cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo 2019
Aidha mshtakiwa aliiomba Mahakama iweze kumpunguzia adhabu kwa kuwa anaishi na bibi yake ambaye anamtegemea
Hata hivyo upande wa mashtaka imeiambia mahakama kuwa ili kukomesha vitendo hivyo mshtakiwa anatakiwa kupewa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine.