Highlands FM

Nyuma ya uwanja: Unyanyasaji wa wanawake wacheza mpira

17 November 2026, 1:10 pm

Vicky Lopez wa Barcelona akiwa uwanjani{Picha Google}

Wanawake wachezaji wa mpira wa miguu wanakabiliwa na changamoto za ukatili wa kijinsia, unyanyasaji, ubaguzi na vitisho vinavyoweza kuathiri maendeleo yao katika soka.

Na Mwanaisha Makumbuli

Licha ya wanawake kujitokeza kushiriki katika mchezo wa mpira wa miguu, baadhi yao wanakabiliwa na changamoto za ukatili wa kijinsia, unyanyasaji, ubaguzi na vitisho vinavyoweza kuathiri maendeleo yao katika mchezo huo.

Changamoto hizo hujitokeza katika mazingira mbalimbali, ikiwemo wakati wa mazoezi, mashindano na hata nje ya uwanja, hali inayozua maswali kuhusu usalama na haki za wanawake katika soka.

Faraja omary  ni mchezaji wa mpira wa miguu amesema kuwa wanakutana na mazingira yasiyo rafiki yanayoweza kuwakatisha tamaa na kudhoofisha ndoto zao za kufanikiwa katika mchezo huo.

Sauti mchezaji wa kike

Kwa upande wake, Zera Steven, ambaye ni kocha, amesema kuwa anahakikisha wachezaji wake wanapata ulinzi na mazingira salama wakati wa mazoezi na mashindano ili kuwawezesha kutimiza malengo yao katika soka.

Sauti Zera

Aidha, baadhi ya wanaume wanaoshiriki katika mchezo wa mpira wa miguu wamesisitiza umuhimu wa kuimarisha mifumo ya kupokea na kushughulikia malalamiko ya ukatili wa kijinsia, pamoja na kuwawajibisha wote wanaohusika na vitendo hivyo.

Sauti ya mwanaume

Hivyo, ni muhimu kwa taasisi zinazosimamia mchezo wa mpira wa miguu kuimarisha hatua za kupambana na ukatili wa kijinsia ili kuhakikisha wanawake wanapata haki, heshima, ulinzi na fursa sawa katika mchezo huo.