Highlands FM

Waziri nanuaka na wasanii wa bongo fleva wawafariji waathirika wa mafuriko mbeya

6 November 2026, 11:23 pm

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Dkt. Joel Nanauka akiwa na baadhi ya viongozi wa jiji la mbeya pamoja na wasanii wa Bongo Fleva {Picha na Samwel Mpogole}

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Dkt. Joel Nanauka, akiambatana na wasanii wa Bongo Fleva, wametembelea na kutoa misaada kwa waathirika wa mafuriko katika Kata ya Nzovwe, Jijini Mbeya huku Zaidi ya wananchi 90 walioathiriwa na mafuriko hayo wamehifadhiwa katika Shule ya Msingi Nzovwe baada ya nyumba zao kuharibika. Ziara hiyo imelenga kuwafariji waathirika na kuwapatia msaada katika kipindi hiki kigumu

Na Samwel Mpogole

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Dkt. Joel Nanauka, akiambatana na wasanii wa Bongo Fleva, ametembelea na kuwapa pole wananchi walioathiriwa na mafuriko yaliyotokea mwanzoni mwa wiki hii katika Kata ya Nzovwe, Jijini Mbeya, huku wakitoa misaada mbalimbali kwa waathirika hao.

Misaada hiyo imetolewa katika Shule ya Msingi Nzovwe, ambako zaidi ya waathirika 90 wa mafuriko hayo wamehifadhiwa baada ya nyumba zao kuharibiwa na mvua hizo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Dkt. Nanauka amesema Serikali inatambua changamoto zinazowakabili waathirika hao na kupongeza hatua ya wasanii kujitokeza kushirikiana na jamii katika kipindi hiki kigumu.

Sauti ya waziri nanauka
Msanii wa Bongo Fleva

Kwa upande wake, msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Farid Kubanda, maarufu kama Fid Q, amesema msaada huo ni sehemu ya kuguswa na hali waliyonayo wananchi hao, huku akieleza kuwa wasanii wana wajibu wa kutumia nafasi zao kusaidia jamii.

Amesema wasanii hao wapo Jijini Mbeya kwa ajili ya onesho la miaka 30 ya muziki wa Bongo Fleva, linalotarajiwa kufanyika Novemba 7 katika Viwanja vya Eden Highland, na wameamua kutumia nafasi hiyo kufanya jambo la kijamii kwa kuwafariji waathirika wa mafuriko.

Sauti Fid Q

Nao baadhi ya wananchi walioathiriwa na mafuriko hayo wameeleza kufurahishwa na msaada walioupata, wakisema umewapa faraja na kuwasaidia katika kipindi ambacho wanakabiliwa na changamoto za kupoteza makazi na baadhi ya mali zao.

Sauti Wananchi