Highlands FM

Waumini waaswa kusoma neno la Mungu nakufanyakazi kwa bidii

7 July 2025, 11:18 am

Mchungaji Rafael Mwambenja. Picha Samwel Mpogole

Waumini wa dini ya kikristo wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanasoma neno la Mungu ili wawe na uelewa zaidi kuhusu dini yao kwa ufasaha.

Na Samwel Mpogole

Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato wametakiwa kujenga utamaduni wa kusoma Neno la Mungu pamoja na lesoni kila siku, ili kuimarika kiroho na kuwa na uelewa mpana wa maandiko.

Wito huo umetolewa na Mchungaji wa Mtaa wa Mrimarel, Rafael Mwambenja, wakati wa ibada iliyofanyika katika Kanisa la Waadventista Wasabato Songwe.

Amesisitiza kuwa kusoma Biblia na lesoni mara kwa mara humsaidia Mkristo kukua kiimani, kuimarika kimaadili na kuwa na bidii katika kutenda kazi ya Mungu.

Sauti Rafael Mwambenja

Katika hatua nyingine, Mchungaji huyo amewahimiza waumini kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo kwa familia, kanisa na jamii kwa ujumla.

Sauti Rafael Mwambenja 2

Baadhi ya waumini walioudhuria ibada hiyo wameeleza namna walivyoguswa na ujumbe huo, huku wakiahidi kufanya mabadiliko chanya katika maisha yao ya kiroho.

Sauti ya Waumini