Highlands FM

Halmashauri ya wilaya ya chunya yavuka kiwango cha mapato ya ndani

12 September 2023, 11:14

Makusanyo hayo yanaifanya halmashauri hiyo kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato ambalo lilikuwa ni sh.  Bilioni 27.9 katika kipindi cha mwaka 2022/2023

Mwenyekiti wa baraza la madiwani wilaya ya chunya Bosco Mwanginde akitoa taarifa ya mapato ya ndani ya halmashauri . picha na Samwel Mpogole

Na Samwel Mpogole

Zaidi ya shilingi bilioni 29.8 zimekusanywa kama mapato ya ndani na halmashauri ya wilaya ya Chunya katika kipidi cha mwaka wa fedha 2022/23.

Akitoa taarifa kwenye kikao cha kawaida cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Chunya,mwenyekiti wa baraza hilo Bosco Mwanginde amesema kutokana na makusanyo hayo halmashauri imevuka lengo kwa zaidi ya asilimia 106.

Mwenyekiti wa baraza la madiwani Bosco mwanginde

Kwa upandewake Venance Luwagila Afisa uhamiaji wilaya ya chunya ameliomba baraza hilo kutoa elimu kwenye jamii kuhusu elimu  ya kudhibiti wimbi la wahamiaji haramu

Afisa uhamiaji wilaya ya chunya Venance luwagilo

Aidha Lutufyo Mwambungu, Mkuu takukuru wilaya ya chunya, amewasihi madiwani hao kuwa na ushirikiano sambamba na kukagua miradi kwakuwa jamii inaamini kupitia wao hivyo kuto kukagua miradi kunaweza iletea hasara serikali

Mkuu wa takukuru wilaya ya chunya Lutufyo Mwambungu

Katika hatua nyingine Anakleth Michombero Katibu tawala, akimuwakilisha mkuu wa wilaya ya chunya amewapongeza madiwani hao kwakutokuwa miongoni mwa halmashauri tano zilizo kwenye sakata la ubadhilifu wa fedha za uma kupitia mashine za ukusanyaji mapato ambapo amewataka kuendelea kusimamia kwa umakini fedha na miradi katika maeneo yao.

Katibu tawala Anakleth Michombero

Kwaupandewake Eliah Chigoji akimuwakilisha mkuu wa mkoa wa mbeya Juma Homera, amewataka madiwani hao kuhakikisha wanaongeza vyanzo vingine vya mapato ili kuendelea kufanya vizuri zaidi

Mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa mbeya Eliah chigoji

Katika kikao hicho madiwani wameadhimia kurejea katika nafasi ya kwanza kuongoza ukusanyaji mapato katika mkoa wa mbeya sambamba na kuendelea kuvuka lengo kila awamu ili kuwa mfano wa kuigwa katika halmashauri nyingine.