Highlands FM

Viongozi wa dini, wananchi watakiwa kuliombea taifa

2 October 2023, 18:22

Mbunge wa jimbo la Lupa pamoja na viongozi wa dini wakizungumza masuala mbalimbali katika kanisa hilo: Picha Samwel Mpogole

Watanzania na waumini wa dini wametakiwa kuliombea taifa na kumwombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuhakikisha nchi inakuwa ya amani na utulivu.

Na Samwel Mpogole

Watanzania na waumini wa dini ya kikristo wametakiwa kuliombea taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Wito huo umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Lupa  Masache Njelu Kasaka aliposhiriki ibada ya Jumapili katika kanisa la Morovian usharika wa Chunya wilaya ya Chunya mkoa wa Mbeya.

Masache pia  alipokuwa kanisani hapo amechangia fedha kiasi cha shilingi milioni moja kwa ajili ya kusaidia miradi inayotekelezwa katika kanisani hilo.

Sambamba na hayo  amewashukuru waumini wa kanisa hilo na viongozi kwa ujumla kwakuendelea kuliombea taifa kwani maombi ni siraha na nguzo katika taifa na jamii kwa ujumala

Mbunge wa jimbo la lupa Masache Kasala akiwa katika kanisa la Morovian Usharika wa chunya wilaya ya chunya mkoani mbeya :Picha Samwel Mpogole