Highlands FM

RC Mbeya awaonya wananchi wanaopotosha kuhusu chanjo ya polio

22 September 2023, 12:44

Maambukizi ya virusi vya polio ni maambukizi yanayoathiri mfumo wa neva na huweza kusababisha udhaifu wa misuli au kupooza,Ugonjwa huu ni adimu, kwa kuwa chanjo imepunguza uwepo wa virusi hivi katika nji nyingi.

Mkuu wa Mkoa wa mbeya Juma Homera akizindua zoezi la utoaji wa chanjo kwa watoto kuanzia miaka 0-8 katika Mkoa wa Mbeya ; picha na mwandishi wetu

na mwanaisha makumbuli

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya  Juma Homera, amewataka wazazi Mkoani hapa kutowaficha watoto wao ndani ili waweze kapatiwa chanjo ya polio kwa lengo la kujikinga na madhara yatokanayo na ugonjwa huo ikiwemo kupooza, ulemavu na kupelekea kifo.

RC Homera ameeleza hayo wakati akizindua zoezi la utoaji wa chanjo kwa watoto kuanzia miaka 0-8 katika Mkoa wa Mbeya, inayotolewa kwa siku nne kuanzia jana ambapo watoto zaidi ya laki sita wanatarajiwa kupata chanjo

Mkuu wa Mkoa mbeya Juma Homera akielezea chanjo ya polio

Dkt Elizabeth Nyema ni kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, ameeleza namna zoezi hilo litakavyofanyika katika kuwafikia watoto wote mkoani humo, huku baadhi ya wananchi wakieleza juu ya umuhimu wa chanjo ya polio kwa watoto wadogo.

Kaimu mganga mkuu wa Mkoa wa mbeya Dkt Elizabeth Nyema akielezea mkakati na mipango Yao juu ya uchanjaji wa chanjo ya polio

Chanjo hii ya polio imeanza kutolewa hapa Nchini katika mikoa ya Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi, Kigoma na Kagera iliyopo mipakani, baada ya kuibuka upya kwa ugonjwa wa Polio katika Nchi za jirani na Tanzania ikiwemo Malawi na kisa kimoja kikiripotowa hapa Nchini katika Mkoa wa Rukwa

Mtoto akipatiwa chanjo ya polio mkoani Mbeya :picha mtandaoni