Highlands FM

‘Feed the Future’ yatoa mafunzo kwa wakulima wa Mboga na Matunda Mbarali

15 November 2023, 14:58

Na Mawanaisha Makumbuli

Mkuu wa wilaya ya mbarali Denisi Mwila akizungumza na baadhi ya wakulima katika kijiji cha Mapunga kata ya igurusi wilayani mbarali.

Na Mwanaisha Makumbuli

Shirika lisilo la kiserikali feed the future wakishirikiana na USAD kutoka nchini marekani wamewapatia mafunzo  wakulima wa mboga mboga na matunda namna bora ya kulima kilimo chenye tija katika mikoa ya Njombe, Morogoro ,Iringa na  Mbeya.

Mkurugenzi wa mradi wa USAD kilimo tija ANTONIO COELLO amesema kuwa mradi huo umewafikia wakulima na vikundi mbalimbali  namna ya kulima kilimo chenye tija ambapo baadhi yao waliweza kufanya vizuri kupitia mradi huo.

Sauti ya antonio coello

Naye mkuu wa wilaya ya mbarali Denisi mwila akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mbeya  amesema kuwa mradi wa kilimo tija  umetoa mchango madhubuti katika kutekeleza muunganiko kati ya wadau mbalimbali huku mafanikio yakionekana kwa wakulima kupitia mradi huo.

Sauti Denisi mwila
Baadhi ya wakulima ambao walipata fursa ya kudhulia mkutano huo;Picha na Mwanaisha Makumbuli

Akizungumza kwa niaba ya wakulima fanueli zakayo mahaye amemewataka wadau hao kuendelea kutoa mafunzo kwa wakulima ili waweze kulima kilimo chenye tija na kuwatafutia masoko nje ya nchi licha ya changamoto wanazopitia kwa sasa juu ya kuuza mazao yao kwani yamekuwa yakiharibika kutokana na kukosa kwa soko.

Sauti ya fanueli zakayo kwa niaba ya wakulima

Kilimo ni mojawapo ya shughuli za mwanadamu ambayo humsaidia kupata mazao kwa ajili ya chakula na mazao mengine kwa ajili ya biashara ambayo inaweza kumuingizia kipato kwa ajili ya maisha yake, pia kipato hicho husaidia katika kukuza uchumi wa nchi yake.