Highlands FM

Maabara ya madini Chunya

13 September 2023, 16:39

Hii hi maabara ya upimaji wa sampuli mbalimbali za madini ,minelabs iliyopo Halmashauri ya wilaya ya chunya mkoani Mbeya

kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Abdala Shaib Kaim akiweka jiwe la msingi kwenye maabara ya madini minelabs . :Picha na #samweli mpogole

Mwanahabari : samweli mpogole

Zaidi ya shilingi milioni 900 zimetumika kujenga miundombinu ya maabara ya upimaji wa sampuli za madini (Minelabs) katika halmashauri ya wilaya ya Chunya.

Mkurugenzi wa kampuni inayosimamia maabara hiyo Simon Shinshi ameueleza msafara wa mbio za mwenge kitaifa kuwa mradi huo umelenga kuongeza thamani kwenye shughuli za uchimbaji wa madini na uzalishaji.

Simon shinshi

Naye kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Abdala Shaib Kaim ameipongeza kampuni hiyo kwa utekelezaji wa mradi huo akieleza kuwa utaongeza pato la taifa ikiwa ni pamoja na kuongeza ajira Kwa wananchi.

Abdala shaib kaim

Aidha, kiongozi hiyo wa mbio za mwenge kitaifa ameridhia,kuweka jiwe la msingi kama ishara ya uzinduzi wa mradi huo.Mwenge wa uhuru unakamilisha ziara ya siku saba katika halmashauri za mbeya kwa kutembelea miradi mbali mbali ambapo baada ya kukamilisha ziara katika wilaya ya chunya utakabidhiwa katika mkoa wa tabora kuendelea na ziara yake hapa Nchini.

kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Abdala Shaib Kaim akikamilisha kuweka jiwe la msingi kwenye maabara ya madini minelabs . :Picha na #samweli mpogole