Highlands FM

Wanafunzi marufuku mikesha ya ngoma(sherehe) za usiku

27 September 2023, 13:07

Afisa tarafa wa sisimba jijini mbeya John mboya akitoa maelekezo kwa wanafunzi kuzingatia masomo wawapo darasani na kuto jihusisha na mambo ya sherehe ;Picha na Samwel Mpogole

Baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwahusisha watoto wadogo kwenye sherehe hali inayopelekea watoto kubadilika tabia na wengine kushindwa kuendelea na masomo na kuwa wanenguaji katika sherehe hizo.

Na Samwel Mpogole

Afisa Tarafa wa Sisimba Jijini Mbeya John Mboya amewataka wazazi na walezi kata ya Itagano Jijini Mbeya kuzingatia suala la elimu na kutowaruhusu wanafunzi kushiriki kwenye sherehe za usiku lakini pia kukemea utoro katika baadhi ya shule zinazopatikana  ndani ya kata hiyo.

Hayo ameyaeleza akiwa katika ziara zake za kupitia na kukagua hali ya taaluma katika kata hiyo  na kugundua kuwepo kwa utoro na wazazi kutosimamia suala la elimu kwa watoto wao hali inayoweza kupelekea kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi.

Sauti ya afisa Tarafa sisimba John Mboya

Pia ametoa rai kwa wanafunzi hao kuhakikisha wanafuatilia masomo yao vizuri ili waweze kutimiza ndoto zao lakini pia amewataka wazazi kuhakikisha wanawafatilia watoto wao katika masomo yao.

Sauti John Mboya wito kwa wazazi

Ziara hiyo inalenga  kutatua changamoto zilizopo katika suala la elimu kata ya  Itagano iliyopo Tarafa ya Sisimba  na kuzungumza na watumishi waliopo katika kata hiyo.

Afisa tarafa sisimba John Mboya ;Picha na Samwel Mpogole