Highlands FM

Jeshi la polisi Mbeya lawataka wanandoa hasa wanaume kutoa taarifa za ukatili

22 September 2023, 12:21

Kamanda wa polisi Mkoa wa mbeya Benjamin Kuzaga: picha mtandaoni

Ukatili ni hali ya kusababisha kwa makusudi mateso na kukosesha raha dhidi ya mtu mwingine, ilihali suluhisho la wazi linapatikana kwa urahisi.

Na Mwanaisha Makumbuli

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Benjamin Kuzaga amesema kuwa jeshi la polisi kupitia dawati la jinsia limekuwa likitoa msaada kwa jamii hususani wanandoa kuhakikisha wanaepuka na vitendo vya ukatili

Akizungumza na Highlands Fm radio, Kuzaga amesema kuwa watendaji waliokuwa kwenye dawati ya kijinsia wameweza kupata elimu ya namna ya kuisaidia jamii ili kuondokana na masuala ya ukatili wa kijinsia.

Kamanda wa polisi mkoani wa Mbeya Benjamin Kuzaga

Aidha kamanda Kuzaga amesema wamekuwa wakishirikiana na ustawi wa jamii ili kutokomeza vitendo vya ukatili vinavyofanywa na baadhi ya wanandoa hasa wanaume ambao wamekuwa wakifanyiwa vitendo hivyo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Benjamin Kuzaga