Highlands FM

CCM Mbeya wajipanga kumpokea Dk.Tulia

4 November 2023, 17:39

Mbunge wa mbeya mjini,spika wa bunge la Tanzania , Raisi wa umoja wa wabunge Dunia (IPU) Dk Tulia acksoni :picha mwandishi wetu

Mwandishi samweli ndoni

Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mbeya imempogeza Spika wa Bunge Dk. Tulia Acksoni kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa umoja wa wabunge duniani (IPU).Dk, Tulia ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini alichaguliwa kuwa Rais wa umoja wa wabunge Duniani (IPU) kwenye uchaguzi uliofanyika Oktoba 27, 2023 jijini Luanda nchini Angola akiongoza kwa kupata kura 172.

Akizungumza na vyombo vya habari, mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa, (CCM) Ndele Mwaselela ambaye ni msimamizi wa vikao vya Chama kwa sasa amesema wameandaa utaratibu wa kumpokea Dk. Tulia.

Anasema “CCM,imeandaa utaratibu wa kumpokea ambao tutashirikiana na wilaya zote wakiongozwa na wilaya ya Mbeya mjini siku ya Novemba 11, 2023, akitokea jijini Dodoma lakini tunampongeza kwa namna alivyokwenda kusimama na kuheshimisha ile azma ya mh. Rais kwamba spika wa bunge atokee Tanzania’’

Mwaselela ameongeza kwakusema ‘’Tunawakaribisha watu wote kuja kumpokea bila kujali vyama vyao, siasa au namna yoyote ile, kwa kuwa Spika amezaliwa na Chama Cha Mapinduzi lakini ni mtoto wa watu wote bila kujali itikadi’