Highlands FM

DC Mbeya awatoa hofu wananchi uhaba wa mafuta

11 September 2023, 17:01

mkuu wa wilaya ya mbeya mh.beno malisa pamoja na Meneja wa wa EWURA Mkoa wa Mbeya Dickson Semkuyu wakikagua mafuta kwenye kituo cha mafuta mkoani mbeya . picha na samweli mpogole

Kumekuwa na hofu kubwa kwa watanzania juu ya uhaba wa mafuta nchini ,hofu kubwa kupanda kwa bei ya nauli endapo kutakuwa na na uhaba wa mafuta nchini

by samweli mpogole

Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mh Beno Malisa amewatoa hofu wakazi wa wilaya ya Mbeya kutokana na kuwepo kwa taarifa ya uhaba wa mafuta katika baadhi ya maeneo mkoani Mbeya.

Akitembelea katika baadhi vituo vya mafuta jijini Mbeya na halmashauri ya wilaya ya Mbeya (Mbeya DC) huku akiambatana na meneja wa wa EWURA mkoa wa Mbeya Dickson Semkuyu, Mh. Malisa amejionea hali halisi ya upatikanaji wa huduma ya mafuta na kubainisha kuwa hapatakuwa na changamoto kubwa ya uhaba wa mafuta na kuwataka wafanyabishara, watumiaji wa vyombo vya moto na wakazi wa Mbeya kuwa watulivu huku jitihada za dhati zikichukuliwa kutatua changamoto hiyo.

hapatakuwa na changamoto kubwa ya uhaba wa mafuta na kuwataka wafanyabishara, watumiaji wa vyombo vya moto na wakazi wa Mbeya kuwa watulivu huku jitihada za dhati zikichukuliwa kutatua changamoto hiyo