Highlands FM

Wazazi waonywa kuwaozesha watoto kwa wachimba madini Chunya

7 November 2023, 19:05

Wanafunzi wa kidato Cha nne shule ya sekondari sangambi wilayani chunya wakiwa kwenye Maafari ya kumaliza kidato Cha nne : picha na samweli mpogole

Na Samweli Mpogole

Wazazi na walezi wilaya ya Chunya wametakiwa kuacha tabia ya kuwafanyisha kazi watoto katika shughuli za uchimbaji madini na kuwaozesha wakiwa bado masomoni badala yake wawasimamie katika masomo yao.

Wito huo umetolewa na Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Ramadhani Shumbi katika mahafali ya kumaliza kidato cha nne yaliyofanyika katika shule ya sekondari Sangambi wilayani humo ikiwa ni mahafali ya kwanza tangu kuanzishwa shule hiyo mwaka 2018.

Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya chunya Ramadhani Shumbi : picha samweli mpogole

Shumbi amesema licha yakuwepo mikakati mbalimbali kuhakikisha shule zilizopo katika halmashauri hiyo zinawekewa mabweni kwa watoto wakike na wakiume amesema bado serikali haitofumbia macho vitendo viovu na vyakikatili vinavyo fanyika katika eneo hilo

Kwa upande wake Diwani wa kata ya sangambi Junjulu Mhewa amesema yeye kama diwani ataendelea kupigania mahitaji kwa wanafunzi na walimu katika shule ya sangambi ili izidi kufanya vizuri kila mwaka.

Diwani kata ya sangambi Junjulu Mhewa : picha samweli mpogole

Ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) imeeleza kwamba vitendo vya ndoa za utotoni vimeendelea kupungua duniani ingawa upunguzaji huo hauna kasi ya kutosha kufikia lengo la kutokomeza ndoa za utotoni ifikapo mwaka 2030 kama yalivyo Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu, SDGs.