Highlands FM

Shule mpya wilayani Chunya kuwakomboa wanafunzi

4 January 2024, 14:07

Mbunge wa jimbo la lupa wilayani chunya mkoani mbeya Masache Kasaka akiwa kwenye mkutano wa adhara na wananchi wa jimbo hilo. Picha na Samweli Mpogole

Tayari tumekwisha Jenga vyumba 8 vya madarasa, ofisi za walimu mbili, jengo la utawala, maktaba, jengo la kompyuta na maabara tatu ya kemia, fizikia na biolojia

Na Samwel Mpogole

Shule mpya ya Sekondari ya Kata Kambikatoto wilaya ya Chunya Jimbo la Lupa  Mkoa wa Mbeya inayotarajiwa rasmi kuanza masomo muhula wa kwanza January inakwenda kuwakomboa wanafunzi kwa kufuata elimu umbali mrefu wa km 98 kutoka Kambikatoto Mpaka Isangawana, Hali iliyokuwa inachangia wanafunzi kuacha masomo, utoro na mimba za utotoni na baadhi ya Wazazi kushindwa kumudu gharama.

Mbunge wa jimbo la lupa wilayani chunya mkoani mbeya Masache Kasaka akiwa kwenye mkutano wa adhara na wananchi wa jimbo hilo. Picha na Samwel Mpogole

Afisa mtendaji Kata Nicholous Ndongosya  ametoa taarifa kwa Mbunge wa Jimbo Masache Kasaka kuwa tayari wamekwisha Jenga vyumba 8 vya madarasa, ofisi za walimu mbili, jengo la utawala, maktaba, jengo la kompyuta na maabara tatu ya kemia, fizikia na biolojia.

Sauti Afisa Mtendaji wa kata

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo la Lupa  Masache Kasaka ameishukuru serikali ya Rais Samia Suluhu Hassani kwa kuendelea kutoa fedha za miradi inayokwenda kutatua changamoto za wananchi.

Sauti Mbunge wa Jimbo la lupa Masache Kasaka

Wazazi ambao ndio walikuwa sehemu ya  waathirika  kwa kukosekana kwa shule katika eneo lao wamesema baadhi yao iliwalazimu kuwasihi watoto wao wafanye vibaya katika mitihani  Ili  kukwepa gharama za kuwapeleka mbali na makazi Yao kupata elimu.

Sauti za Wazazi