Highlands FM

Wananchi jijini Mbeya wakanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni tatizo la maji

11 September 2023, 12:50

Picha ya maji yakitoka kwenye bomba . Picha kwa njia ya mtandao

Kumekuwa na mkanganyiko juu ya upatikanaji wa maji baadhi ya maeneo mkoani Mbeya hasa kipindi hiki cha kiangazi kitendo kinachopelekea baadhi ya wananchi kulalamika kukosekana kwa maji.

Na Samweli Ndoni

Baadhi ya wananchi wa kata za Isanga na Iganzo wamekanusha taarifa iliyosambaa mitandaoni ikidai kuwa maeneo yao kuna tatizo kubwa la maji, taarifa ambayo si kweli bali changamoto wanazozipata ni za kawaida ambazo zipo katika maeneo yote hasa katika msimu huu wa kiangazi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema kumekuwa na utaratibu wa mgawo wa maji ambao wananchi wote wanafahamu na walitangaziwa na mamlaka husika kwamba baada ya siku mbili maji lazima yatoke.

Sauti ya Mwasapila Alphosi

Diwani wa kata ya Iganzo ameweka wazi changamoto waliyokuwa wanaipata kuwa ilitokana na kupasuka kwa bomba la maji na tayari kazi inaendelea ya kulihamisha bomba hilo ili wananchi waendelee kunufaika na huduma ya maji.

Sauti ya diwani

Kutokana na kadhia hiyo uongozi wa kata ya Iganzo umewataka wananchi kutosikiliza taarifa zisizo sahihi kuhusu maendeleo ya eneo hilo.

Sauti ya kiongozi