Highlands FM

UWSA kula sahani moja na watumishi waomba rushwa

7 November 2023, 13:50

Mkurugenzi Mtendaji wa Mbeya akizungumza na wananchi wa mji mdogo wa Mbalizi.

Na Samweli Ndoni

Uongozi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jiji la Mbeya (Mbeya-UWSA) umetangaza kula sahani moja na watendaji wazembe ikiwemo wale wanaojihusisha na vitendo vya kuwaomba rushwa wateja ili wawape huduma.

Hatua hiyo imetangazwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mbeya-UWSA, CPA Gilbert Kayange wakati akisiliza kero za wananchi katika mamlaka ya mji mdogo Mbalizi.

CPA Kayange ameonya kuwa mamlaka itawashughulia watendaji wote wanaofanya Kazi zao kinyume na miongozo ya mamlaka ikiwemo wale wanaoomba Rushwa Kwa wateja.

Baadhi ya wananchi wametoa kero na ushauri kupitia mkutano wa hadhara ambapo pamoja na mambo mengine wameipongeza mamlaka Kwa kuboresha huduma Katika mji mdogo wa Mbalizi.