Highlands FM

Wananchi wa ilembo halmashauri ya wilaya ya mbeya waondokana na adha ya umeme

9 October 2023, 13:39

Mkuu wa wilaya ya mbeya Benno Malisa akizungumza na baadhi ya wananchi wa kata ya ilembo ;Picha na Samwel Mpongole

Serikali ya Tanzania imekuwa ikitekeleza miundombinu katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo elimu ambapo wanafunzi wamekuwa wakipata elimu na kutimiza ndoto zao

Na Samweli Mpogole

Wananchi wa Kata ya Ilembo Halmashauri ya Wilaya Mbeya wameishukuru Serikali kwa Kuwafikishia huduma ya Umeme pia kuwajengea Sekondari ya Wasichana ya Pareto  

Shukrani hizo zimetolewa  mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Beno Malisa alipo tembelea Katika kata hiyo Ili kuona Maendeleo ya ujenzi  wa shule ya wasichana Pareto na kusikiliza kero za wananchi wa kata hiyo ambapo  Wananchi waliibuka na kutoa hisia zao Juu ya kile kilichofanywa na Serikali l.

Hata hivyo wameendelea kusema  kuwa Serikali imefanya jambo muhimu  kuwashirikisha wadau Ili kusaidia Ujenzi wa Shule ya wasichana itakayosaidia wasichana waliopo katika kata hiyo kutotembea umbali mrefu kufuta huduma ya elimu 

Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbeya  amesisitiza Wakazi wa Ilembo na Halmashauri ya Wilaya Mbeya kushirikiana ipasavyo na Makampuni  yanayojihusisha na ununuzi wa zao la Pareto ambao waliahidi Kuchangia Katika ujenzi wa Shule hiyo haraka iwezekanavyo.

Aidha Malisa amewasisitiza Wakazi wa Ilembo kuwa wavumilivu Kwakuwa  Serikali yao ni Sikivu na itendelea kuwapelekea maendeleo katika maeneo hayo ikiwemo kuboresha Miundombinu ya Barabara na Maji.