Highlands FM

‘Jizingatie’ kuwanusuru vijana na maambukizi ya Ukimwi

16 December 2023, 16:26

Baadhi ya wanafunzi pamoja na vijana mkoani mbeya wakipatiwa mafunzo namna ya kujikinga na maambukizi ya viruzi vya Ukimwi.

Na Prince Fungo

Mwandishi wa Habari

Highlands Fm radio

Tanzania  inaweza kufikia lengo la kuondokana na maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi ifikapo mwaka 2030 ikiwa wananchi watatambua umuhimu wa kupima afya zao.

Pia wamesisitizwa ili kufikia lengo hilo la kimkakati ni lazima wachukue  taadhari ikiwemo kuepuka ngono zembe.

Hayo yamejiri wakati shirika lisilokuwa la kiserikali HJMRI kwa kushirikiana na taasisi ya afya ckeck  wakizindua mpango wa jizingatie ambao umelenga kuhamasisha wananchi hasa vijana wenye umri kuanzia 15 hadi 24 kupima na kujilinda.

Akitoa maelezo wakati wa zoezi hilo kwenye viwanja vya Luanda nzovwe jijini Mbeya mratibu wa kambi za afya check Dr. Isaac Maro Amesema kuna umuhimu wa wananchi kupima afya zao ili kusaidia kwenye mapambano dhidi ya  Ukimwi.