Highlands FM

Mapogoro walia kukosa huduma ya mawasiliano

2 October 2023, 17:55

Baadhi ya wananchi wakielezea changamoto zinazowakabili kijijini hapo. Picha Mwanaisha Makumbuli

Kukosekana kwa mawasiliano ya kutosha kunapelekea baadhi ya wananchi hasa waishio vijijini kushindwa kuwasiliana na ndugu zao pamoja na uzalishaji mali kudorola na kushindwa kufikia malengo yao.

Na Mwanaisha Makumbuli

Baadhi ya wanakijiji wa Mapogoro halmashauri ya wilaya ya Chunya mkoani Mbeya wameiomba serikali kuwatatulia kero mbalimbali zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa huduma ya  mawasiliano ya simu.

Wakihojiwa kwa nyakati tofauti baadhi ya wanakijiji hao wamesema ukosefu wa mawasiliano unapelekea washindwe kuwasiliana na jamaa zao hivyo kulazimika kwenda maeneo mengine ili kupata huduma hiyo.

Changamoto nyingine waliyoielezea ni pamoja na gharama ya usafiri wa bajaji ambayo imekuwa adha kwa wanakijiji hao.

Sauti za wananchi kijiji cha Mapogoro

Naye mwenyekiti wa kijiji hicho amesema changamoto zote zilizoelezwa na wananchi zinajulikana na serikali inaendelea kuzitafutia ufumbuzi..

Sauti Mwenyekiti wa kijiji Geogre Ngululo
Picha ;Mwanaisha Makumbuli