Highlands FM

Vitambulisho vya taifa zaidi ya 360,000 vyafika mkoa wa Mbeya

29 November 2023, 10:39

Mkuu wa mkoa wa Juma Homera akizungumza na wananchi wa kata ya isuto kuhusu ugawaji wa vitambulisho vya Nida.

Na Samwel Mpogole

Mkuu wa mkoa wa mbeya Juma Zuberi  Homera amefanya uzinduzi wa wa zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya Taifa (NIDA) huku akiwataka wakuu wa wilaya wote kufanya uzinduzi huo kwenye wilaya zao.

Uzinduzi huo umefanyika Novemba 27/2023 katika kata ya Isuto halmashauri ya wilaya mbeya huku ukishuhudiwa na viongozi mbali mbali wa halmashauri hiyo akiwemo mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Mbeya Vijijini Ndg. Ackimu Sebastiani Mwalupindi.

Homera katika uzinduzi huo pia amewasisitiza viongozi wa kata kuhakikisha wanagawa vitambulisho hivyo vyote kwa wahusika kwani wananchi wamekuwa wakivisubiri kwa muda mrefu.

Hata hivyo  amemshukuru Rais Dkt. Samia kwakuwapatia vitambulisho hivyo zaidi ya 360,000 katika mkoa wa mbeya huku halmasya wilaya ya Mbeya ikiongoza kupata vitambulisho vingi.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa mbeya Juma Homera

Mkuu wa mkoa wa mbeya Juma Homera akikabidhi kitambulisho cha nida kwa mwananchi wa kata ya isuto.
Mkuu wa wilaya ya Mbeya Benno Malisa akizungumza na wananchi wa kata ya isuto iliyopo jiji mbeya